Arusha, Tanzania : 23 Aprili, 2018: KUNDI la wataalamu wanaotekeleza mradi wa kimataifa wenye lengo la kuongeza uzalishaji wandizi k...
Arusha, Tanzania
: 23 Aprili, 2018:
KUNDI la
wataalamu wanaotekeleza mradi wa kimataifa wenye lengo la kuongeza uzalishaji
wandizi kwa nchi za Uganda na Tanzania, wanakutana mjini Arusha wiki hii, kwa
nia ya kutathmini maendeleo ya mradi huo na kupanga shughuli zinazotakiwa
kufanyika mwakani.
Wataalamu hao
wanaofanya utafiti wa migomba watakutana kuanzia tarehe 23 hadi 27 Aprili
katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST)
iliyopo mjini Arusha.
Ndizi ni zao la
chakula na pia chanzo kikuu cha mapato kwa mamilioni ya wakulima wadogo wa
migomba katika nchi za i Tanzania na Uganda. Mataifa haya mawili ndiyo
yanayozalisha nusu ya ndizi zinazozalishwa barani Afrika zenye thamani ya Dola
za Marekani Bilioni 4.3 kila mwaka.
Hata hivyo
wakulima hao kwa sasa wanazalisha asilimia 9 tu ya uwezo wao wa uzalishaji
kutokana na athari za wadudu na magonjwa yanayokumba zao hilo.
Mradi huo
wauzalishaji wa mbegu bora ya migomba umelenga kuwapelekea wakulima mbegu bora
ya migomba yenye kuzaa zaidi na kukabiliana na magonjwa .
Mbegu hiyo
inatarajiwa kuipita mbegu inayotumika sasa katika uzalishaji kwa zaidi ya
asilimia 30 kwa mazingira yaleyale.
Mradi huo
umejikita zaidi katika kufanikisha kuendelea kuwapo kwa aina mbili za mbegu
ambazo ni maarufu kwa ukanda huo, Matooke na Mchare ambayo hulimwa sana nchini
Tanzania.
“Mradi huu wa
uzalishaji wa mbegu bora umejikita zaidi kuwapatia wakulima mbegu wanayoipenda
na yenye kuhimili matatizo ya msingi ya sasa. Hata hivyo, ni vigumu sana kupata
miche ya migomba aina inayotakiwa kutokana na zao hilo kutokuwa na mbegu au
punje. Wazalishaji mbegu wanapata mbegu kwa kutumia mgomba wenyewe na mchakato
wake huchukua muda mrefusana,” anasema Profesa RonySwennen, mzalishaji kiongozi
wa migomba katika Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Kilimo katika kanda ya
Tropiki (IITA) ambaye pia ni Mtafiti kiongozi wa mradi huo.
“Watafiti katika
mradi huu wanafanya kazi pamoja kwa kutumia utaalamu wa kisasa zaidi katika
maabara zetu duniani kote ilikukabiliana na changamoto za uzalishaji wa mbegu
hizi, kuharakisha mchakato wake wauzalishaji na kuongeza uzazi wa aina mpya ya
miche ya migomba yenye kuzaa zaidi na kuhimili magonjwa nawadudu,” alisema
Profesa Rony Swennen.
Mradi huo
unawaleta pamoja watafiti waandamizi wa migomba kutoka nchi za Australia, Ubelgiji,
Brazil, Jamhuri ya Czech, India, Kenya, Malaysia, Afrika Kusini, Sweden,
Tanzania, Uganda naMarekani.
Mradi huo ambao
sasa uko katika mwaka wa tatu, umewezesha Tanzania kwa mara ya kwanza kuwa na
programu ya kuzalisha migomba na mbegu ya kwanza ya ndizi Mchare iliyofanyiwa
kazi kwak uunganishwa na migomba poriy enye uwezo mkubwa wa kuhimili magonjwa,
umepandwa mwaka huu 2018. Uzalishaji wa mbegu za Matooke upo katika ngazi za
juu na kwamba zaidi ya miche 250 ya Matooke iliyofanyiwa utafiti imechaguliwa
kufanyiwa majaribio nchini Uganda na Tanzania.
Magonjwa ambayo
yanatazamwa sana ni mnyauko na Sigatoka nyeusi ya migomba na upande wa wadudu
ni minyoo (au kwa kitaalamu parasitic nematodes ) na wadudu wanaokula migomba
ambao ni fukuzi (au kwa kitaalamu Weevils).
Uzalishaji huo wa
mbegu bora unaenda sambamba na utafiti wa kuelewa ukubwa wa kiwango cha
uharibifu na kusambaa kwa wadudu na magonjwa hayo na kutengeneza mfumo wa
haraka wa kutambua magonjwa na kuzalisha mbegu ambazo zinahimili changamoto
hizo.
Katika mradi huu
imebainika pia kwamba ugonjwa wa Sigatoka unasambaa katika maeneo mengine na
huenda ni kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Ili mradi huo
uwezekuwa endelevu,pia unawafunza watafiti wa baadae wa migomba kwa kuwapatia
nyenzo mpya za ufundi na utaalamu wa kisasa wa uzalishaji wa mbegu bora za
migomba.
Pia mradi unatoa
nafasi ya kubadilishana vinasaba vya migomba kati ya nchi na maabara
tofauti kwa ajili ya utafiti na kutumia kinasaba bora kwa ajili ya kutengeneza
mbegu mpya, ikianzisha ushirikiano wa kimataifa wa mfumo wa uzalishaji wa
migomba duniani.
Mradi huo
unaoongozwa na kuratibiwa na IITA kwa ushirikiano na wadao wengi nchini
Tanzania na Uganda.
Shughuli ya
uzalishaji wa mbegu hiyo mpya ya migomba inafanyika katika Taasisi ya Sayansi
naTeknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) Arusha, Tanzania kwa ushirikiano
wa karibu na Taasisi za Utafiti wa Kilimo nchini Tanzania (ARI) katika maeneo
yanayozali shandizi; na Programu ya uzalishaji wa migomba kwenye Taasisi ya
Taifa ya Utafiti wa kilimo ya Uganda (NARO) katika maabara za Kawanda na
Sendusu, mjini Kampala.
Mradi huu
unaendeshwa kwa mujibu wa taratibu za utafiti za CGIAR za mazao ya mizizi na
ndizi (RTB).
COMMENTS